Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kutoka kushoto) amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika uwanja wa michezo wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) ambao utatumika kwa mazoezi wakati wa mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu ya CHAN 2025 na AFCON 2027. Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 29 Oktoba, 2024 aliambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipata ufafanuzi kuhusu mchoro wa uwanja wa michezo kutoka kwa Afisa Miliki wa LST, Bw. Saddam Salim alipofanya ziara katika Taasisi kwa ajili ya ukaguzi wa uwanja huo unaotarajiwa kufanyiwa ukarabati hivi karibuni ili uweze kutumika kwenye mazoezi ya mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu ya CHAN 2025 na AFCON 2027. Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 16 Septemba, 2024 aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi (wa pili kutoka kulia).
Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan akizungumza katika mhadhara wa kitaaluma kutoka kwa Wataalamu wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi tarehe 30 Aprili, 2024 katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (The Law School of Tanzania).
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria wa kipindi hicho, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya LST, Menejimenti na Wahitimu wa Kozi ya Astashahada ya Wasaidizi wa Kisheria katika mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi tarehe 27 Machi, 2024.
Wanafunzi wa Law School wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo
Baadhi ya wahitimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) wakila kiapo cha Uwakili mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania.