Majukumu ya Taasisi
Majukumu ya Taasisi
Majukumu ya msingi ya Taasisi yameainishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Taasisi Sura ya 425 ambayo ni:
-
Kutoa, kuendesha na kusimamia mafunzo ya unasheria kwa vitendo chini ya usimamizi wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini (the Council of Legal Education).
-
Kuweka mazingira na miundombinu itakayowezesha utoaji elimu ya uanasheria kwa vitendo
-
Kuendesha mitihani na kuwatunukia vyeti wahitimu wa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo.
-
Kudhamini, kupanga, kutoa vifaa kwa ajili ya kuendesha semina, makongamano na mikutano katika masuala yanayohusu sheria
-
Kutoa machapisho mbalimbali ya shughuli zinazohusiana na Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi
-
Kufanya tafiti za kisheria kwenye maeneo mahsusi kama itakavyoamuliwa na Bodi ya uendeshaji ya Taasisi.
-
Kutumia matokea ya tafiti hizo kuboresha mafunzo ya uanasheria kwa vitendo, fasihi na uboreshaji wa mtaala na ufundishaji.
-
Kutoa ushauri elekezi kuhusu masuala ya kisheria kwa Serikali, umma na taasisi binafsi, na kwa mtu mmoja mmoja ndani na nje ya nchi
-
Kutangaza machapisho mbali mbali ambayo yanatokana na kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi kama itakavyoamuliwa na Bodi ya uendeshaji ya Taasisi
-
Kudhamini na kutoa vifaa kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji ya ndani na umma.
-
Kuanzisha ushirikiano na vyuo na taasisi zingine zote za kitaifa na kimataifa
-
Kufanya shughuli nyingine za kisheria kama itakavyoekelezwa na Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi.