Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mhe. Hamza Johari (katikati) akishuhudia makabidhiano ya hati ya makubaliano ya kuimarisha mashirikiano baina ya Ofisi yake na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST). Hafla hiyo imefanyika tarehe 2 Julai, 2025 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno na kulia ni Mkuu wa Taasisi ya LST Prof. Sist Mramba.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania - Divisheni ya Kazi, Mhe. Jaji Dkt. Yose Mlyambina amekabidhi juzuu za maamuzi ya migogoro ya kazi kwa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST). Juzuu hizo zimepokelewa na Mkuu wa Taasisi ya LST, Prof. Sist Mramba na zinatarajiwa kuwasaidia wanafunzi, watafiti na wadau mbalimbali wa masuala ya sheria kupata rejea sahihi na tafsiri za kisheria katika migogoro ya kazi. Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 10 Oktoba, 2025 katika Ofisi za LST jijini Dar es Salaam ambapo yalishuhudiwa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu pamoja na LST.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi (katikati) akiimba wimbo wa wafanyakazi pamoja na viongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa LST lililofanyika tarehe 3 na 4 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Homera (aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa na Menejimenti pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) alipotembelea LST kwa ziara ya kikazi tarehe 12 Desemba, 2025. Katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri Mhe. Zainab Katimba pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula.
Wanafunzi wa Law School wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo
Baadhi ya wahitimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) wakila kiapo cha Uwakili mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania.