WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. BALOZI DKT. PINDI CHANA ATEMBELEA LAW SCHOOL.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametembelea Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) tarehe 12 Septemba, 2023 kwa lengo la kufahamiana na Watendaji wa Taasisi pamoja na kupata uelewa kuhusu majukumu ya Taasisi hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Pindi alipata fursa ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya Taasisi ikiwemo jengo linalotumika kufundishia wanafunzi, ofisi za Watumishi pamoja na jengo la maktaba.
Aidha alizungumza na Watumishi wa Law School kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji pamoja na kutoa nasaha zake kwa wanafunzi aliowakuta madarasani wakijisomea. Katika ziara yake Mhe. Balozi Dkt. Pindi pia aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mary Makondo pamoja na Watendaji wengine kutoka wizarani.