Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST)

lst Logo
Mawakili Wapya Wasisitizwa Kuzingatia Maadili ya Taaluma
01 Dec, 2023
Mawakili Wapya Wasisitizwa Kuzingatia Maadili ya Taaluma

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Juma amewaasa mawakili wapya 279 kuzingatia maadili na weledi katika taaluma yao kwa kuwa mambo hayo ndio msingi wa kazi zao.

Jaji Mkuu aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika sherehe za 69 za kuwapokea na walikubali mawakili hao ambapo kati yao wanawake ni 118 na wanaume ni 169 ambao kwa pamoja wanaongeza idadi ya mawakili nchini kutoka 11,637 hadi kufikia 11,916.

"Mnapaswa kuzingatia maadili ya taaluma yenu kwa sababu tendo la wakili mmoja kukiuka maadili linaweza kuchafua taswira ya soko la ajira za mawakili wa Tanzania kwa kuwa linaweza kutumika kama mfano mbaya," alisema Prof. Juma.

Pia alisisitiza kuwa kama ilivyo kwa majaji na mahakimu, mawakili ni taaluma inayoheshimika sana hivyo vitendo, kauli na myenendo yao yote iwe ya heshima kwa sababu wakiruhusu mihuri yao kutumiwa vibaya itapunguza hadhi na heshima ya uwakili.

Aidha, Jaji Mkuu aliwataka mawakili hao kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani kwa kuwa taaluma ya sheria haiwezi kukwepa mapinduzi ya viwanda ambayo tayari yameshaingia mahakamani.

"Tumeanza kujifunza utaratibu mpya wa kuratibu na kusimamia mashauri mahakamani kwa njia ya mtandao, mfumo huu ni muhimu sana, umekuja kuchukua nafasi ya mfumo uliokuwepo awali. Mfumo huu una faida nyingi kubwa kuliko changamoto ambazo tunazitumia kujiimarisha," alieleza.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi aliwataka mawakili hao kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali wanapotekeleza majukumu yao kwa sababu wao ni maafisa wa mahakama hivyo wamepewa dhamana ya kuisaidia Mahakama katika utoaji haki kwa wakati.

"Kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya mawakili wa kujitegemea kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutohudhuria mahakamani, kutotunza siri za mteja, kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya wakili na mteja, kutumia mihuri isivyo halali na mengine mengi. Hayo yote ni ukiukwaji wa sheria kanuni na maadili ya taaluma hii,” alisisitiza Dkt. Feleshi.

Naye Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST), Prof. Sist Mramba aliwapongeza mawakili hao wapya kwa kuapishwa na kusema kuwa mawakili hao ni zao la Taasisi hiyo. 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
https://saris.lst.ac.tz/Registrations

" >